logo trf

MASHAMBULIZI YA MTANDAONI DHIDI YA WANAHABARI: FAHAMU HAKI ZAKO NCHINI KENYA

Contents

Unaathiriwa na aina ipi ya unyanyasaji wa mtandaoni?

threats icon

VITISHO

 • Vitisho vya kiuhalifu hujumuisha vitisho vya kifo, vitisho vya kubakwa, au vitisho vya vurugu vinavyofanywa mtandaoni. Vitisho vya mtandaoni vinaweza kuchukuliwa kama unyanyasaji wa mtandaoni chini ya Kifungu cha 27 cha Sheria kuhusu Uhalifu wa Mtandaoni na Matumizi Mabaya ya Kompyuta (Computer Misuse and Cyber Crimes Act), Kipengee cha 5 cha 2018. Wewe au wakili wako mnaweza kuomba mahakama zimshurutishe mtu yeyote anayetoa vitisho vya mtandaoni kukoma.
 • Kanuni ya Adhabu (Penal Code) pia inashughulikia aina fulani za vitisho vya mtandaoni: vitisho vya kuua mtu (Kifungu cha 223), kutumia vitisho kuitisha mali (Kifungu cha 299), na vitisho vya kuchoma mali ya mtu (Kifungu cha 344). Una haki ya kupiga ripoti kwa polisi.
brigading icon

KUHOFISHA

 • Kuhofisha kunajumuisha vitendo vinavyomtisha au kumtia mtu hofu. Kuhofisha mtandaoni kunaweza kuchukuliwa kama unyanyasaji wa mtandaoni chini ya Kifungu cha 27 cha Sheria kuhusu Uhalifu wa Mtandaoni na Matumizi Mabaya ya Kompyuta, Kipengee cha 5 cha 2018. Wewe au wakili wako mnaweza kuomba mahakama zimshurutishe mtu yeyote anayetoa vitisho vya mtandaoni kukoma.
 • Kifungu cha 238 cha Kanuni ya Adhabu kinapiga marufuku matukio ya kuhofisha, na kuyabainisha kuwa tukio lolote lenye nia ya kusababisha taharuki au kumfanya mtu asichukue hatua fulani (k.m. kuchapisha taarifa fulani); au kitendo chochote kinachosababisha au kinachonuia kusababisha madhara kwa mtu, hadhi yake, mali yake au mtu anayehusiana naye (yaani, rafiki, mwanafamilia, nk.). Una haki ya kupiga ripoti kwa polisi.
 • Vifungu vya ziada vya Kanuni ya Adhabu vinaweza pia kutumika: vitisho vya kuua (Kifungu cha 223), kutumia vitisho kuitisha mali (Kifungu cha 299), na vitisho vya kuchoma mali ya mtu mwingine (Kifungu cha 344). Una haki ya kupiga ripoti kwa polisi.
cyberstalking icon

KUNYATIA MTANDAONI

Kunyatia mtandaoni ni matumizi yanayorudiwa ya mawasiliano kupitia mbinu za kielektroniki ili kumlenga mtu kwa njia isiyofaa au ya uvamizi. Sheria ya Kenya haifafanui tukio la kunyatia mtandaoni kwa njia mahususi. Hata hivyo, linaweza kurejelewa chini ya:

 • Kifungu cha 27 cha Sheria kuhusu Uhalifu wa Mtandaoni na Matumizi Mabaya ya Kompyuta, Kipengee cha 5 cha 2018, ambacho kinapiga marufuku unyanyasaji wa mtandaoni. Tukio hili linajumuisha mwenendo ambao unaweza kusababisha wasiwasi kwa mtu au hofu ya vurugu kwake au ya uharibifu au ya kupoteza mali yake; hali ambayo humdhuru mtu, au hali ambayo haionyeshi heshima au ambayo inakera sana. Una haki ya kuomba mahakama zimshurutishe mtu yeyote anayehusika katika matendo ya unyanyasaji wa mtandaoni kukoma.
 • Kifungu cha 238 cha Kanuni ya Adhabu, ambacho kinapiga marufuku matukio ya kuhofisha. Hali hii inaweza kutumika katika matukio ya kunyatia mtandaoni iwapo unaweza kuonyesha: nia ya kukutia hofu; nia ya kukufanya uchukue hatua fulani au kuacha kuchukua hatua fulani (k.m. kuchapisha taarifa fulani); kuwa inakufanya wewe au mtu unayehusiana naye kupata madhara; au inaleta madhara kwa hadhi yako, mali yako au ya mtu unayehusiana naye. Iwapo vipengee vyovyote kama hivyo vinapatikana katika tukio linalokuathiri la kunyatia mtandaoni, una haki ya kupiga ripoti kwa polisi.
 • Kifungu cha 223 (vitisho vya kuua), kifungu cha 299 (vitisho vya kupeana mali) au kifungu cha 344 (vitisho vya kuchoma mali yako) katika Kanuni ya Adhabu. Iwapo vipengele vyovyote kati ya hivi vinapatikana katika tukio linalokuathiri la kunyatia mtandaoni, una haki ya kupiga ripoti kwa polisi.
doxxing icon

KUCHAPISHA TAARIFA ZA SIRI

 • Tukio la Kuchapisha Taarifa za Siri ni shambulizi la mtandaoni linalohusu kuchapisha taarifa za mtu kwenye intaneti bila idhini yake. Sheria ya Ulinzi wa Data, Kipengee cha 24 cha 2019, inapiga marufuku uchakataji usio halali wa data ya kibinafsi. Taarifa zako za siri zikichapishwa, una haki ya kuwasilisha malalamiko kwa Kamishna wa Data.
 • Kifungu cha 37 cha Sheria kuhusu Uhalifu wa Mtandaoni na Matumizi Mabaya ya Kompyuta, Kipengee cha 5 cha 2018, kinapiga marufuku usambazaji wa picha za siri (kwa kawaida tukio hili hufahamika kama “ponografia ya kulipiza kisasi”). Iwapo mtu amesambaza picha zako za siri bila idhini yako, una haki ya kuomba mahakama zimshurutishe akome.
 • Kifungu cha 31 cha Katiba kinahakikisha haki ya kulinda faragha. Ulinzi huu unajumuisha haki ya kuzuia taarifa za kibinafsi au mawasiliano ya faragha yasifumbuliwe bila sababu inayofaa. Iwapo taarifa zako za siri zimechapishwa, una haki ya kuwasilisha mashtaka kwa mujibu wa katiba kwa Mahakama Kuu ukiiomba itekeleze haki hii.
 • Iwapo uchapishaji huu wa taarifa za siri unaathiri hadhi yako vibaya, una haki pia ya kuwasilisha mashtaka dhidi ya kashfa (defamation) katika mahakama ya madai (civil court). Sheria kuhusu kashfa nchini Kenya hutekelezwa tu katika kesi za madai.
impersonation icon

KUIGA MTU MTANDAONI

 • Iwapo mtu ametumia au anatumia saini yako ya kielektroniki, nenosiri lako, au kipengee kingine chochote cha kukutambulisha, basi una haki ya kuwasilisha mashtaka ukiomba mahakama zimshurutishe anayefanya hivyo kukoma, kwa mujibu wa Kifungu cha 29 cha Sheria kuhusu Uhalifu wa Mtandaoni na Matumizi Mabaya ya Kompyuta, Kipengee cha 5 cha 2018. 
 • Iwapo mtu ametumia au anatumia jina lako au jina, jina la biashara, chapa ya biashara, jina la kikoa, au neno au kauli nyingine unayomiliki au unayotumia, bila idhini inayofaa, basi una haki ya kuwasilisha mashtaka ukiomba mahakama zimshurutishe anayefanya hivyo kukoma, kwa mujibu wa Kifungu cha 28 cha Sheria dhidi ya Uhalifu wa Mtandaoni na Matumizi Mabaya ya Kompyuta, Kipengee cha 5 cha 2018.
trolling icon

UCHOKOZI

 • Uchokozi unahusu kutoa kimakusudi maoni yanayokera au kuudhi mtandaoni. Sheria ya Kenya haifafanui tukio la uchokozi kwa njia mahususi. Hata hivyo, sheria na kanuni zinazofafanua matukio ya unyanyasaji, vitisho au kuhofisha, zinaweza kutumika kwenye matukio ya uchokozi. Tafadhali tumia vifungu vilivyo hapo juu vinavyofafanua kwa kina njia tofauti unazoweza kutumia, kulingana na tukio la uchokozi ambalo limekukumba au linakukumba.
 • Kulingana na hali ya uchokozi, hatua za kuchukua zinaweza kujumuisha kupiga ripoti kwa polisi, kuwasilisha mashtaka mahakamani ya kumshurutisha anayefanya hivyo akome, na/au kumshtaki katika mahakama ya madai kwa kusababisha madhara.
brigading icon

UVAMIZI

 • Uvamizi huhusu unyanyasaji uliopangwa kwa kumshambulia mtu au jamii kupitia maoni mengi ya kuchochea. kuchukiza na/au kupotosha. Sheria ya Kenya haifafanui tukio la uvamizi kwa njia mahususi. Hata hivyo, sheria na kanuni zinazofafanua matukio ya unyanyasaji, vitisho au kuhofisha, zinaweza kutumika kwenye matukio ya uvamizi. Tafadhali tumia vifungu vilivyo hapo juu vinavyofafanua kwa kina hatua mbalimbali unazoweza kuchukua, kulingana na tukio la uvamizi ambalo limekukumba au linakukumba.
 • Kulingana na hali ya uvamizi, hatua za kuchukua zinaweza kujumuisha kupiga ripoti kwa polisi, kuwasilisha mashtaka mahakamani ili kumshurutisha anayefanya hivyo akome, na/au kuwashtaki katika mahakama ya madai kwa kusababisha madhara.
 • Sheria kuhusu Hatia za Kingono, Kipengee cha 3 cha 2006, inapiga marufuku unyanyasaji wa kingono, unaobainishwa kama matendo ya kingono yasiyotakikana yanayofanywa na mtu aliye mamlakani au afisa wa umma ambaye anatarajiwa kufahamu kuwa matendo hayo hayaruhusiwi na mwathiriwa. Iwapo umeathiriwa na tukio la unyanyasaji wa mtandaoni unaohusisha matendo ya kingono yasiyotakikana na anayefanya hivyo ni afisa wa umma, una haki ya kupiga ripoti kwa polisi.

Nitachukua hatua gani iwapo anayetekeleza unyanyasaji hajulikani?

Ingawa sheria za Kenya hazifafanui tukio la unyanyasaji unaotekelezwa na mtu usiyemfahamu kwa njia mahususi, kuna hatua mbalimbali unazoweza kuchukua ili kujaribu kumtambua anayefanya hivyo:

 • Kuwasilisha malalamiko kwa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (Directorate of Criminal Investigations) na kuwapa machapisho yoyote ya mtandaoni yanayofaa kama ushahidi.
 • Kupiga ripoti kuhusu unyanyasaji unaotekelezwa na mtu usiyemfahamu kwa Timu ya Kitaifa ya Kenya ya Kushughulikia Matukio ya Kompyuta – Kituo cha Kuratibu (National Kenya Computer Incident Response Team – Coordination Center). 

 

Bila kujali idara ambako unapiga ripoti au kuwasilisha malalamiko haya, idara hizi zitashirikiana kukusanya ushahidi. Baada ya kukamilisha kukusanya ushahidi, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai itaelekeza kesi hiyo kwa Ofisi ya Msimamizi wa Mashtaka ya Umma (Office of the Director of Public Prosecutions) ili aanze mchakato wa kuwafungulia wahusika mashtaka.

Nitachukua hatua gani iwapo unyanyasaji unajumuisha asili ya rangi na/au jinsia?

remember the alt text
REUTERS/ Damir Sagolj

Sheria kuhusu Uwiano na Uadilifu wa Kitaifa, Kipengee cha 12 cha 2008, inapiga marufuku ubaguzi au unyanyasaji kwa misingi ya kabila.  Iwapo unakumbwa na aina yoyote ya unyanyasaji kwa misingi ya kabila lako, unaweza kuwasilisha malalamiko kwa Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Uadilifu.

Sheria kuhusu Uwiano na Uadilifu wa Kitaifa pia inapiga marufuku matamshi ya chuki, ambayo yanafafanuliwa kama uchapishaji au usambazaji wa nyenzo za matusi na yananuiwa kusababisha chuki ya kikabila. Iwapo umeathiriwa na tukio la matamshi ya chuki, una haki ya kuwasilisha malalamiko kwa Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Uadilifu.

Kifungu cha 27 cha Katiba kinampa kila mtu haki ya usawa na uhuru dhidi ya ubaguzi wa aina yoyote. Iwapo unaathiriwa na aina yoyote ya unyanyasaji unaohusu ubaguzi kwa misingi ya rangi na/au jinsia yako, wewe (au wakili wako) una haki ya kuwasilisha mashtaka kikatiba kwa Mahakama Kuu ukiomba itekeleze haki hii.

Nitachukua hatua gani iwapo unyanyasaji unafanywa na mtu aliye katika nchi nyingine?

Hatia kwa mujibu wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandaoni na Matumizi Mabaya ya Kompyuta, Kipengee cha 5 cha 2018, (CMCA, Computer Misuse and Cyber Crimes Act) ambayo imefanyika nje ya Kenya itachukuliwa kuwa imefanyika nchini Kenya iwapo mtu anayefanya au kukosa kufanya kitendo hicho ni raia wa Kenya au anaishi Kenya; na hali ya kufanya au kukosa kufanya kitendo hicho inamlenga raia wa Kenya. Katika tukio hili, mamlaka za Kenya zitakuwa na haki chini ya sheria ya CMCA ya kutekeleza wajibu wake bila kujali kama kosa hilo lilifanyika nje ya Kenya.

REUTERS/Andrew Kelly

Nitachukua hatua gani kama shirika la habari, au mfanyakazi wa shirika la habari, anayenyanyaswa mtandaoni?

Kama shirika la habari, unaweza pia kuathiriwa na unyanyasaji wa mtandaoni. Mifano ya matukio ya unyanyasaji wa mtandaoni ambayo yanaweza kukumba shirika la habari ni pamoja na – lakini si tu – kashfa, vitisho na kuhofisha. Iwapo shirika lako limeathiriwa na tukio la kiuhalifu la unyanyasaji wa mtandaoni, una haki ya kupiga ripoti kwa polisi.

Iwapo mwanahabari aliyeajiriwa ameathiriwa na tukio la unyanyasaji wa mtandaoni, hatua za kisheria unazoweza kuchukua ni chache. Madai mengi ya unyanyasaji wa mtandaoni yanapaswa kuwasilishwa na mwanahabari mwenyewe. Vyumba vya Habari vinahimizwa kutoa mwongozo unaowafahamisha wafanyakazi kuhusu hatua za kisheria wanazoweza kuchukua iwapo wataathiriwa na tukio la unyanyasaji, na kuwapa usaidizi wa kukusanya ushahidi na, wakipenda, kuwasilisha malalamiko.

Kagua ufahamu wako!

Dodoso hili fupi la hiari linaweza kutumiwa kukadiria ufahamu wako kuhusu sheria kuhusu unyanyasaji wa mtandaoni nchini Kenya baada ya kusoma ukurasa huu.

Pakua Mwongozo wa Kenya wa Kufahamu Haki Zako (Know Your Rights Guide).

Some crimes can be prosecuted but require the victim (or a representative of the victim) to file a criminal complaint in order to begin prosecution proceedings against the perpetrator(s). If you are a victim of such a crime (or the representative of one) you have six months from the time the perpetrator(s) are identified to file a criminal complaint and request that they be prosecuted.

Some crimes require the government, represented by the Public Prosecutor’s Office, to prosecute the alleged perpetrator(s) whether or not the victim presses charges. Crimes of this nature are subjected to what is called unconditional public prosecution. If you are a victim of a crime subjected to unconditional public prosecution and have reported the crime, no further immediate action is required on your part in order to ensure the perpetrator(s) are prosecuted.

Some crimes give both the government and the victim the option to press charges against the perpetrator(s). They do not, however, require the government to step in and prosecute as crimes subject to unconditional public prosecution do. If you are a victim of such a crime, you have six months from the date it is committed against you to request the state pursue charges against the perpetrator(s). The government, represented by the Public Prosecutor’s Office, also has six months to file charges against alleged perpetrator(s) whether or not the victim requests it. If you are a victim of a crime that is subject to conditioned public prosecution and wish to see the perpetrator(s) prosecuted, you will need to be proactive in requesting that charges be filed and/or following up with the Public Prosecutor’s Office to ensure they file charges and begin prosecution proceedings.

Skip to content